Rais wa kundi la Waasi wa M23, Bertrand Bisimwa amewataka Waandishi wa Habari waache kusambaza kile alichokiita uzushi kuwa M23 inaungwa mkono na Rwanda akisema hizo ni propaganda za Viongozi wa DRC kuwalaumu Rwanda kwa makosa yao wenyewe ndani ya Nchi ya Congo.
Akiongea na Waandishi wa Habari Bisimwa amesema Rais wa Congo Tshisekedi anapaswa kufikishwa Mahakamani kwa kosa la kuwaingiza Watoto wadogo kwenye vikundi vya Jeshi ili washiriki vita inayoendelea akisema hatua hiyo inafanya Vijana wadogo wapoteze maisha.