Mahakama ya Kisutu Yashindwa Kutoa Uamuzi Kesi ya Dr Slaa

Mahakama ya Kisutu Yashindwa Kutoa Uamuzi Kesi ya Dr Slaa


Japokuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilitarajia kutoa uamuzi leo, Januari 31,2025 kwenye shitaka linalomkabili Dkt. Wilbroad Slaa, ikiwa ni baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuagiza shauri la Dkt. Slaa lirejeshwe Kisutu kwaajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake, uamuzi umeshindwa kutolewa

Kwa mujibu wa Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki, uamuzi huo umekwama baada ya Jamhuri kukata Rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa hivyo wanafungwa mikono katika uamuzi mpaka majibu ya rufaa hiyo yatakapotolewa

Aidha, kufuatia uamuzi huo baada ya mabishano ya Kisheria, Wakili upande wa Mshtakiwa, Peter Madeleka ameeleza kuwa yeye na timu ya mawakili wengine wa utetezi hawajaridhishwa na maamuzi hayo kwani uwepo wa rufaa bado hauzuii haki zingine za msingi za mshatakiwa kama kupatiwa dhamana

#JamiiForums 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad