Makamo Mwenyekiti Chadema John Heche Amtembelea Dr Slaa Gerezani...




Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mheshimiwa John Heche, leo amefanya ziara maalum kumtembelea Dr. Wilbrod Slaa katika Gereza la Keko jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo iliwashirikisha viongozi kadhaa wa CHADEMA, wakiwemo Bi Rose Mayemba, mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu wa Kanda ya Serengeti, pamoja na viongozi wengine akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Songwe, Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara, na Ndg. Odero, aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Katika mazungumzo yao, Dr. Slaa alitoa pongezi kwa uongozi mpya wa CHADEMA akiwatakia kila la heri katika kutekeleza majukumu yao.

Pongezi hizi zimechukuliwa kama ishara ya matumaini na mshikamano, hasa kutokana na mchango mkubwa wa Dr. Slaa katika historia ya chama hicho na siasa za Tanzania.

Ziara hii imekuja wakati ambapo suala la Dr. Slaa linaendelea kufuatiliwa kwa karibu na wanachama wa CHADEMA pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Kwa kauli fupi lakini yenye matumaini, ujumbe wa “Mbele Kuna Mwanga” umetajwa kuwa kiashiria cha imani kwa mustakabali mzuri wa chama na taifa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad