Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara limefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani Watuhumiwa wawili ambao ni Mapacha, Danford Steven Seif (24) na Daniel Steven Seif (24) wote Wakulima na Wakazi wa Mraushi A’ Wilaya ya Masasi Mkoani humo kwa tuhuma za mauaji ya Upendo Methew Mayaya (42) ambaye ni Mama yao mzazi.
Taarifa iliyotolewa leo January 13,2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara SACP Issa Suleiman, imesema “Watuhumiwa hao walitekeleza kitendo hicho December 15, 2024 kwa kumpiga Mama yao katika paji la uso kwa kutumia jembe na mwichi na kumsababishia majeraha yaliyopelekea kifo chake, chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina”