Ahmed Arajiga na Frank Komba ni miongoni mwa marefa 63 walioteuliwa katika orodha ya awali ya waamuzi watakaofanyiwa mchujo wa kuchezesha fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) 2024 zitakazofanyika kuanzia Februari Mosi hadi Februari 28 mwakani katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.
Orodha hiyo ya awali ina marefa wa kati 25, waamuzi wasaidizi 22 na marefa 16 watakaokuwa wakisimamia teknolojia ya video ya usaidizi kwa marefa (VAR).
Arajiga ambaye ni refa bora wa Ligi Kuu Tanzania msimu uliomalizika, anaingia katika kundi la marefa wa kati huku Komba aliyekuwa refa bora msaidizi wa Ligi msimu wa 2022/2023 amewekwa katika orodha ya marefa wasaidizi.
Katika kundi la marefa 25 wa kati, mbali na Arajiga kuna Messie Nvoulou, Bito Frank, Malala Yannick, Ouattara Jean, Kpan Franklin, Abdulsalam Abiola, Adissa Ligali, Aklesso Linama, Melki Mehrez, Loutfi Bekouassa, Ahmed Mahmoud, Ahmed Abdulrazg, Kech Mustapha, Rakotojaona Andofetra, Milazare Patrice, Celso Alvacao, Jelly Chavani, Mohamed Athoumani, Nyagrowa Mimisa, Lucky Kasalirwe, Mogos Tsegay,Jammeh Lamin, Diouf Adalbert na Ousmane Diakhate.
Marefa wasaidizi 22 ni Komba, Ngila Bongele, Rodrigue Mpele, Malondi Yanes, Addy Dodoo, Oumar Sanou, Samuel Pwadutakam, Yacouba Aziz, Nassiri Hamza, Adel Abane, Wael Hanachi, Amaldine Soulaimane, Lucky Kegalogetswe, Mutuyimana Dieudonne, Fasika Yehualashet, Omer Ahmed, Emery Niyongabo, Mwangi Kuria, Ronald Katenya, Joel Doe, Diba Hamedine na Jawo AbduAziz.
Katika teknolojia ya VAR, marefa walioteuliwa ni Kabore Vincent, Abou Coulibaly, Brahamou Sadou, Boukhalfa Nabil, Hamza El Fariq, Haggag Ibrahim, Badi Luxolo, Ngakosso Chancelle, Nguiene Pierre, Brighton Chimene, Abdalaziz Ahmed, Dintwa Keabetswe, Twagimurukiza Abdoul, Sarr Ababacar na Diou Moussa.
Mchujo huo utafanywa na wakufunzi watano ambao miongoni mwao kuna wajumbe wa kamati ya marefa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) ambao ni Adjovi Alain, Mohammed Guezzaz, Janny Sikazwe, Evarist Menkouande, Mohamed Ali na Boubaker Hannachi.
Fainali za Chan mwakani zitashirikisha timu 18 ambazo ni Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Sudan, Nigeria, Angola, Madagascar, Zambia, DR Congo, Congo, Afrika ya Kati, Burkina Faso, Niger, Mauritania, Senegal, Guinea na Morocco.