Maria Sarungi Adaiwa Kutekwa Kenya na Watu Wenye Silaha


Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linasema kwamba mwanaharakati na mhariri wa kujitegemea kutoka Tanzania Maria Sarungi ametekwa nyara akiwa nchini Kenya.

Katika taarifa kupitia mtandao wa X, shirika hilo limesema kwamba Maria alitekwa na wanaume watatu waliokuwa na silaha na ambao walikuwa na gari nyeusi aina ya Noah.
Aidha limeongeza kuwa kisa hicho kimetokea mwendo wa saa tisa na robo mchana katika eneo la Chaka Place, mtaa wa Kilimani mjini Nairobi.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Irungu Houghton amesema kuwa wako katika eneo la tukio wakijaribu kupata taarifa zaidi.

Credit | BBC Swahili

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad