Maria Sarungi Afunguka Aliyopitia Mikononi Mwa Watekaji Kenya....




Akizungumza na Wanahabari, leo Januari 13, 2025 #MariaSarungi amesema amesema alikamatwa na Watu wanne ambao walimfunga pingu, walimfunika uso na kumkalia wakitaka nywila (password) za simu zake ambazo walifanikiwa kuondoka nazo

Amesema “Naamini dhamira yao ilikuwa kupata vifaa vyangu kama simu na kuingia katika akaunti zangu za Mitandaoni ikiwemo kuchunguza shughuli zangu ninazofanya Mitandaoni. Waliniambia wananipeleka nje ya Nairobi, kuelekea Mpakani.”

Aidha, Maria amesema kuwa wakati wanamuachilia walimwambia asigeuke nyuma wala kuongea na mtu yeyote na wanamuangalia

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad