Idadi ya vifo kutokana na moto wa nyika huko Los Angeles nchini Marekani imeongezeka hadi kumi na sita (16), ikiwa ni kulingana na mchunguzi wa matibabu wa LA.
Kumi na mmoja (11) wamefariki katika moto wa Eaton karibu na Pasadena na watano katika moto wa Palisades huku wafanyakazi wakihangaika kuzuia moto huo kutoendelea kuenea na kuzunguka jiji hilo.
Ndege za kumwaga maji zimekuwa zikifanya kazi usiku kucha kujaribu kudhibiti maeneo ya moto, huku upepo mkali ukirejea ambao ulisababisha uharibifu mkubwa wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa kituo cha BBC, moto mkubwa zaidi ni ule wa Palisades, ambao ni 11% na unawaka kwa kipande cha ekari 23,654, ikiwa ni kulingana na Cal Fire. Moto huo unatishia eneo la watu matajiri la Brentwood na maeneo mengine mashuhuri.
Na wa pili kwa ukubwa ni moto wa Eaton kaskazini mwa jiji karibu na Pasadena, unaofunika ekari 14,118 ambapo 15% umedhibitiwa.
Moto wa Kenneth umeenea ukubwa wa ekari 1,052 na 90% tayari umedhibitiwa, wakati moto wa Hurst ukienea ukubwa wa ekari 799 huku 76% ukidhibitiwa.