Mbowe : Tumekuwa na Ugumu Mkubwa wa Kuendesha Chama Kwa Miaka Saba
"Tulianza kufanya shughuli za Chama Tarehe 4, Machi 2023 baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kwamba lile zuio haramu la kuzuia vyama vya siasa kufanya kazi zake limeondolewa pale ndipo tulianza kukipanga Chama upya.
"Tulijikuta katika kipindi kigumu sana cha miaka miwili kukipanga Chama chetu kuanzia ngazi ya Vitongoji kule chini mpaka kufika ngazi ya Taifa, tukajikuta ndani ya Serikali za Mitaa, huku tukifanya chaguzi ndani ya Chama na mwaka huu tuna uchaguzi mkuu na kwa sababu tunajua kalenda ya sheria ya vyama vya siasa inatulazimisha lazima tupate viongozi wapya ili Chama kiwe halali"- Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA