Niishukuru sana familia yangu, kwa namna ambavyo kwa muda wote wa utumishi wa chama hiki, kwakweli walinivumilia sana, hata leo matokeo yalipotoka, mtu wa kwanza kunipigia simu alikuwa binti yangu, baadaye akanipigia mama yake, nikaongea nao, nikampa simu Lissu akazungumza na mke wangu, kwasababu kihistoria sisi ni marafiki wa kifamilia, ni familia, mama akashukuru akasema maliza haraka baba njoo nyumbani nikupikie supu. WanaCHADEMA wenzangu kakiendelezeni hiki chama pale tulipoishia sisi, ninawaomba WanaCHADEMA wote, viongozi wote wa makundi yote, wasaidieni viongozi hawa (Wakiongozwa na Tundu Lissu) kwasababu wanachokiongoza siyo mali yao, wanaongoza taasisi ambayo wote sisi ni wadau, na Watanzania wote ni wadau, basi tushikamane ili chama hiki kiwe na kesho iliyokuwa bora zaidi"- Mbowe.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa Freeman Mbowe akizungumza mara baada ya Tundu Lissu kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho siku ya Jumatano Januari 22, 2025 katika Mkutano Mkuu wa CHADEMA uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam.