MBOWE: Uchaguzi Ukimalizika Kamati Kuu Itaamua Hatua Gani Imchukulie Tundu Lissu

MBOWE: Uchaguzi Ukimalizika Kamati Kuu Itaamua Hatua Gani Imchukulie Tundu Lissu


Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @chadematzofficial Taifa Freeman Mbowe na mtia nia wa hiyo, ametoa wito kwa uongozi mpya utakaoingia madarakani baada ya uchaguzi wa chama hicho kuchukua hatua dhidi ya wote waliokuwa wakitoa lugha chafu na na kutukana wengine wakati wa mchakato wa uchaguzi wa chama hicho.


Akifanya mahojiano na Salim Kikeke mtangazaji wa Crown Media Mbowe amesema ”anapotoka kiongozi yoyote ndani ya chama au mwanachama kamtukana kiongozi yoyote ndani ya chama sio lazima Mwenyekiti huko ni kukosa nidhamu na ni vile tu mambo haya yametokea ghafla ni imani yangu tutakapomaliza chaguzi hizi uongozi mpya utakapoingia madarakani lazima ushughulikie jambo hili kwa nguvu kubwa sana”


Mbowe ameongeza kuwa “hakuna uhalali wowote wa mwanachadema iwe ni kiongozi au mwanachama au mpenzi kutoka na kudhalilisha viongozi kutoka na kudhalilisha wanachama wenzake mimi kama mtu ambaye nimekijenga hiki chama kwa uchungu mkubwa nakwazika sana”


Katika kipindi hicho alipoulizwa juu ya kama kwa nini hatua asichukue saivi Mbowe amesema “kwa sababu saivi ukichukua hatua yoyote tafsiri yake ni kwamba unafanya hivi kwa sababu huyu sio wa kundi lako”


Baadae Mbowe aliulizwa kama akishinda je atachukua hatua dhidi ya Makamu wake wa sasa akaeleza kuwa Lissu akishinda ataamua mwenyewe kujichukulia hatua ama lah “kama atajichukulia hatua za kinidhamu ama viongozi wengine wakishachanguliwa wataamua kuchukua hatua dhidi ya mwenyekiti wa wakati huo hayo ni ya kwao” 


Alipoulizwa vipi yeye akishinda hatochukua hatua? akajibu ya kuwa “mimi sifanyi maamuzi peke yangu nafanya maamuzi na kamati kuu yangu kama nitashinda mimi kamati kuu mpya itakuwa imeundwa sasa watakaokuwa viongozi wao ndio watakashughulika na yaliyokuwa yamejiri kwenye kipindi hiki cha uchaguzi ndani ya chama”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad