Toka Yanga ianzee kukaa sawa chini ya Ramovic hii ndio mechi ngumu zaidi kwao, Al Hilal kuna vitu vingi wanavo weza kuwa test Yanga na kujua wapi walipo fikia katika huu ujenzi mpya chini ya Ramovic.
Al Hilal wakiwa na mpira wapo direct kutafuta gapes zilizo achwa na mpinzani na kwakutumia kasi na ufundi wa wachezaji wao hua wanatoa sana adhabu kwa style hio ( kama ilivokua kwa Mkapa Yanga waliruhusu magoli ya namna hio)
Mechi ya leo itatoa majibu bila ya mpira na kwenye mashambulizi ya kushtukiza Yanga wameimarika kiasi gani? Katika mchezo iliopita kiukweli Yanga bila ya mpira bado haijawa ya kuridhisha.
Kuna muda wanampa mpinzani time na space ya kukaa na mpira na kuangalia sehemu gani kuna gape ya kupiga pasi hatari, dhidi ya Tp inawezekana Tp walikosa utayari zaidi lakini vile dhidi ya Al Hilal wanaweza kukuadhibu zaidi.
NAAMANI YANGA WANATIMU YA KUPATA GOLI MBELE YA AL HAIL, NNACHO TAKA KUONA LEO NI BALANCE ZAIDI YA KUSHAMBULIA NA KUZUIA 🙌🏼