"Kifupi baraza lote la vijana limeshikiliwa na watu wanaomuunga mkono Lissu na walifanya interview wakasema wapiga kura wa Baraza la Vijana Chadema wanamtaka Tundu Lissu na hii ilidhihirika wakati uchaguzi pia unafanyika unaona alipoingia Freeman Mbowe namna alivyoshangiliwa na alipoingia Tundu Lissu pia namna alishangiliwa.
Na uongozi wote kuanzia Mwenyekiti wa BAVICHA, Makamu mwenyekiti nae wa BAVICHA na katibu wa BAVICHA wote wanamuunga mkono Tundu Lissu na kwenye wajumbe wa BAVICHA wako 21, hao 20 wote wanamuunga mkono Lissu na mmoja tu ndie anatokea kambi ya Mbowe ameshinda. Baraza la Vijana ni watu walioamua kuchagua mabadiliko" - Gerva Lyenda - Meneja wa Kampeni na Mawasiliano wa Tundu Lissu.