Kipa wa Singida Black Stars, Metacha Mnata amesema msimu huu ameajiri wataalamu watatu wa kumchukua video wakati wa mechi ili kupata urahisi wa kujua kitu gani anapaswa kuboresha katika majukumu yake.
.
“Tangu nianze kufanya kazi na vijana hao ni miezi mitano. Nawalipa kila mwezi. Nimeona faida kubwa katika hilo, kwani hivi karibuni baada ya kumalizika mzunguko wa kwanza nimekaa nao chini na kuanza kupitia mechi moja baada ya nyingine nikagundua napaswa niboreshe kitu gani,” alisema Metacha na kuongeza
.
“Duru la pili naamini nitakuwa na vitu vipya nitakavyoongeza katika kazi zangu. Ukiachana na hilo inanisaidia katika mazoezi binafsi kujua naelekeza nguvu eneo lipi.”
.
Katika mechi 15 za duru la kwanza Metacha anamiliki clean sheet saba na alidaka mechi moja ya Kombe la FA, hivyo alisema mzunguko wa pili utakuwa wa ushindani zaidi kuanzia katika timu hadi mechi.