Tukio linaloendelea kutrend kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, ni la mwanadada mrembo, Linda De Sousa Abreu, askari magereza aliyehukumiwa kifungo cha miezi 15 jela baada ya kukutwa na hatia ya kufanya mapenzi na mfungwa ndani ya selo.
Mfungwa Linton Weirich (36), mkazi wa jijini London, Uingereza.
Mfungwa mwenyewe ni Linton Weirich (36), mkazi wa jijini London, Uingereza ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka minne jela katika Gereza la HMP Wandsworth kwa kosa la wizi wa kuvunja.
Linton alikutwa na hatia ya kuiba mali zenye thamani ya pauni 65,000 za Uingereza baada ya kuvunja ‘safe’ katika nyumba moja iliyopo Kensington nchini Uingereza.
Linda De Sousa Abreu
Miongoni mwa vitu alivyodaiwa kuviiba ilikuwa ni vito vya thamani ikiwemo mikufu, hereni na bangili, laptop na begi lililokuwa na fedha.
Linda alihukumiwa hapo jana kutumikia kifungo cha miezi 15 jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mfungwa huyo gerezani.