Mnyika Amkana Wenje "Fedha za Join The Chain Zilitumika na Chama"

Mnyika Amkana Wenje "Fedha za Join The Chain Zilitumika na Chama"


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ametoa ufafanuzi wa kina kuhusu tuhuma zilizotolewa na Ezekia Wenje, mtia nia wa nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa chama hicho, juu ya kampeni ya Join the Chain, akisisitiza kuwa kampeni hiyo ilikuwa na malengo halali ya kuendesha shughuli za chama.


Mnyika ameeleza kuwa Join the Chain ilikuwa kampeni maalum iliyoanzishwa na CHADEMA kati ya Februari na Mei 2022 kwa lengo la kukusanya fedha za kugharamia shughuli za chama, hususan Mkutano wa Baraza Kuu la Mei 2022.


"Fedha taslimu zilizokusanywa kupitia akaunti za benki na namba za simu zilizotangazwa zilikuwa Shilingi milioni 114, ambazo zilitumika kugharamia sehemu ya Mkutano wa Baraza Kuu. Aidha, mapato yote, ikiwa ni pamoja na ada na kadi za kidijitali, yalifikia Shilingi milioni 371," amesema Mnyika.


Mnyika ameongeza kuwa taarifa za makusanyo na matumizi ya fedha hizo zilitolewa kwa Kamati Kuu katika vikao vitatu tofauti, na matumizi hayo yalipitia ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambapo chama kilipata hati safi.


Akijibu moja kwa moja tuhuma za Wenje, Mnyika amesema:"Majibu sahihi ni kwamba hakuna mjumbe wa Kamati Kuu anayepaswa kusema hafahamu. Kama hajui, basi ama hana mamlaka ya kusemea masuala ya fedha au amesahau takwimu."


Amesisitiza kuwa malengo ya kampeni hiyo yalikuwa wazi na yalitekelezwa kwa uwazi, bila ajenda yoyote ya siri kama inavyodaiwa.


Awali, Ezekia Wenje alidai kuwa kampeni ya Join the Chain ilikuwa na lengo la kuandaa mazingira ya kumuondoa Freeman Mbowe katika uongozi wa CHADEMA, hasa wakati alipokuwa gerezani kwa tuhuma za ugaidi.


"Lengo kubwa lilikuwa kukusanya fedha, kuitisha Baraza Kuu, na baadaye Mkutano Mkuu ili Freeman Mbowe aondolewe kwenye nafasi ya uenyekiti na Tundu Lissu achukue nafasi hiyo," alisema Wenje.


Wenje alieleza kuwa Godbless Lema, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya kampeni hiyo, alihusika moja kwa moja na uendeshaji wa vuguvugu hilo, akidai kuwa fedha za kampeni hiyo hazijulikani zilipo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad