“Lazima afahamu kwamba mimi sio Mfanyakazi wa Serikali, mimi ni Mwakilishi wa Wananchi, mimi ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mtu ambaye anaweza kutoa taarifa na rekodi kwamba sihudhurii vikao kwa mujibu wa sheria ni Bunge na sidhani kama yeye kwa nafasi yake ni sehemu ya Bunge”
“Ule mkutano haukuwa mkutano wa Mkuu wa Mkoa, ile ziara haikuwa ziara ya Mkuu wa Mkoa, ilikuwa ni ziara ya Waziri wa Ujenzi na mimi niliyemuuliza ni Waziri wa Ujenzi nilitegemea yeye ndiye angeweza kutupatia majibu ya changamoto yetu lakini cha kushangaza zaidi nikaona Bwana Makonda ametoa majibu ambayo kimsingi hayakuhusiana na hoja ambazo nimezijenga”
Hiyo ni sehemu ya aliyoyaongea Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo akiongea leo Arusha kumjibu Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda ambaye jana alisema Mbunge huyo haudhurii vikao kama inavyotakiwa.