Habari zilizotufikia hii leo Januari 24, 2025 zimeeleza kuwa presha waliyokuwa nayo familia ya wanandoa Sosthenesi Melkizedeki Mrema na Joana Melkizedeki, wakazi wa eneo la Galagaza wilayani Kibaha katika Mkoa wa Pwani baada ya kuporwa mtoto wao wa miezi 7 na gari aina ya Toyota IST, imeshuka baada ya mtoto huyo kupatikana.
GLOBAL TV ilikuwa ya kwanza kuripoti tukio la kuvamiwa kwa familia hiyo yapata siku nane zilizopita ambapo watu wasiojulikana waliondoka na mtoto na gari kisha kuwatumbukiza wanandoa hao kwenye mashimo ya choo na kufunika.
Taarifa kutoka kwenye familia hiyo zimeeleza kuwa wanandoa hao wachanga waliokuwa na mtoto huyo pekee wapo kwenye taratibu za kupatiwa mtoto wao huyo kutoka kituo cha Polisi.