Namuhitaji Tundu Lissu na Lissu Ananihitaji Mbowe

Namuhitaji Tundu Lissu na Lissu Ananihitaji Mbowe

“Hatuwezi kujenga Chama cha ukombozi katika Nchi hii kama kila mmoja hawezi kumuona mwenzake kama bega la kulilia katika mapambano, sio kweli kwamba kutezwana, kutukanana, kukashifiana, kudhalilishana, kufanyiana character assasination kunaweza kuwa sehemu ya kujenga Chama imara, leo nilikuwa namuuliza Mh. Lissu pale kwamba hawa Vijana hawa wa moto kwelikweli hivi walizaliwa mwaka gani!?, akaniambia Mwenyekiti wakati tunaanzisha CHADEMA hawa hawakuwepo lakini maana yake mmekua na mmekikuta Chama hiki “


“Mmekikuta Chama kwakuwa Watangulizi wenu walipendana, waliheshimiana, walijengana, walipendana, wakapatana wakafanya kazi pamoja, kwa tabia iliyoonyeshwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu sio utamaduni wa CHADEMA, kila mmoja wenu anamuhitaji mwingine, Mimi namuhitaji Lissu, Lissu ananihitaji Mbowe, Mimi namuhitaji Pambalu, Pambalu anamuhitaji Heche, yaani tunahitajiana wote katika umoja wetu kama familia ya CHADEMA”


“Pepo lolote lenye dhana ya kututenganisha hatupaswi kulilea lishindwe kwa nguvu zote, ni kweli tutanyukana lakini tukishanyukana tukimaliza kunyukana, tutaonana kwenye boksi tukimaliza boksi lazima tushikane mikono tutafute njia ya kufanya kazi kwa sababu tunahitajiana”


“Nyinyi mmekikuta Chama, mtakuwa na Watoto, tunataka Watoto wa Watoto wenu wakikute Chama hiki kikiwa imara kuliko jana, kwa lengo la kutukanana na kufarakana tunaiua Taasisi iliyoundwa kwa jasho na damu za Watu hatupaswi kuendekeza, hivi vyeo vinapita malengo yetu ni ya msingi kuliko nafasi zetu” —— Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiongea kwenye Mkutano wa BAVICHA leo January 13,2025

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad