Ndege Yawaka Moto, Abiria 176 Waokolewa

Ndege Yawaka Moto, Abiria 176 Waokolewa


Ndege ya Abiria kutoka Shirika la Air Busan aina ya Airbus A321 imewaka moto katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Gimhae, Busan Nchini Korea Kusini na kusababisha Abiria 176 kuokolewa kwa dharura.

Imeelezwa kuwa moto huo ulianza muda mfupi kabla ya Ndege hiyo kupaa kuelekea Hong Kong ambapo Wizara ya Uchukuzi ya Korea Kusini imethibitisha kuwa Abiria 169 pamoja na Wahudumu saba wa Ndege walilazimika kutumia mabomba ya dharura kuokolewa.

Taarifa ya Mamlaka haijatoa maelezo kuhusu chanzo cha moto huo isipokuwa imethibitisha kuwa ulianzia sehemu ya nyuma ya Ndege, nalo Shirika la Zimamoto la Taifa limeripoti kuwa moto huo ulizimwa kikamilifu huku Watu watatu wakipata majeraha madogo wakati wa uokoaji.

Tukio hili linakuja chini ya mwezi mmoja baada ya ajali mbaya ya Ndege ya Jeju Air aina ya Boeing 737-800 iliyotokea Desemba 29 ambapo Ndege hiyo ililipuka baada ya kugonga kizuizi cha zege katika Uwanja wa Ndege wa Muan na kusababisha vifo vya Watu 179 kati ya 181 waliokuwemo ndani.

Aidha Msemaji wa kampuni ya Airbus amesema wanafuatilia tukio hilo kwa karibu na wako kwenye mawasiliano na Air Busan ili kubaini chanzo cha moto huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad