Klabu ya Simba imetoa mapumziko ya siku nne [4] kwa wachezaji wake na benchi la ufundi baada ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo dhidi ya CS Constantine.
Baada ya hapo nyota hao watarudi kambini kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara na kombe la Shirikisho nchini.