Peter Msigwa, aliyekuwa mbunge wa Iringa na mwanachama wa zamani wa Chadema, amemshambulia Freeman Mbowe kupitia mtandao wa X, akidai kuwa alihusishwa na njama za kumtoa Chadema na kumlazimisha kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Msigwa aliandika ujumbe akisema kuwa "Sinema ilianzia kanda ya Nyasa," akimzungumzia Mbowe na kudai kuwa alichimba shimo kwake, lakini sasa shimo hilo limetumbukia mwenyewe.
Msigwa aliongeza kwa kusema kuwa Mungu huwa anajibu maombi, akionyesha furaha yake kwamba hatimaye alijibu maombi yake na haki kumjia.
Ujumbe wa Msigwa ulilenga kumtupia lawama Mbowe, ambaye aliongoza Chadema kwa kipindi kirefu, na kudai kuwa alikuwa sehemu ya njama za kumtoa katika chama hicho.
Wengi wamekuwa wakikisia kuwa Msigwa aliondolewa Chadema kwa makubaliano ya nyuma ya pazia, huku wengine wakidai kuwa alilazimishwa kujiunga na CCM ili kuendelea na siasa zake.
Msigwa ameonekana kuwa na hasira kutokana na matukio yaliyomkuta, huku akionyesha kuwa anafurahi kwa kuona Mbowe akishindwa katika uchaguzi wa chama hicho.
Ujumbe wa Msigwa umeibua mjadala mzito kuhusu uongozi wa Chadema, huku wengi wakiwa na maswali kuhusu mchakato wa uchaguzi na uongozi wa Mbowe katika chama hicho.