Rais Mteule Donald Trump Aapishwa Marekani...



Rais Mteule Donald Trump ameapishwa rasmi hii leo January 20,2025 kuwa Rais wa 47 wa Marekani katika hafla iliyofanyika katika jengo la Bunge (Capitol Hill) Mjini Washington.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Trump kurejea katika Ikulu ya Marekani kwa kipindi cha miaka minne baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwezi November mwaka jana na anachukua nafasi ya rais Joe Biden anayeondoka Ikulu hii leo ikiwa ni miezi miwili na nusu baada ya kumshinda Makamu wa Rais anayemaliza muda wake Kamala Harris katika uchaguzi mkuu.

Awali sherehe ya uapisho ilipangwa kufanyika katika eneo la siku zote nje ya Bunge la Marekani lakini zimehamishiwa ndani kwa sababu ya hali ya hewa katika Jiji la Washington.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad