Rais Samia Awateua Viongozi Watano Serikalini


Rais Samia Awateua Viongozi Watano Serikalini


Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mhandisi Ramadhani Masoud Lwamo kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini ambapo kabla ya uteuzi huu, Lwamo alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Rais Samia amemteua pia Dkt. Aggrey Kalimwage Mlimuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ushindani (FCC) kwa kipindi cha pili na pia amemteua Prof. Othman Chande Othman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kipindi cha pili.

Wengine walioteuliwa na Rais Samia ni Dkt. Florens Martin Turuka ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kwa kipindi cha pili na Prof. Valerian Cosmas Silayo ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini(CAMARTEC) kwa kipindi cha pili.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad