Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Yanga SC baada ya ushindi dhidi ya TP Mazembe.
Kupitia mtandao wake wa kijamii ameandika-: "Hongera kwa Klabu ya Yanga kwa ushindi dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika"
"Nawatakia kila la kheri katika michezo iliyosalia kwenye mashindano haya. Endeleeni kutupa burudani na kufanya kazi njema ya kuipeperusha vyema bendera ya nchi yetu kimataifa" Rais Samia