Shabiki wa yanga Fanya Chochote ili Yanga Ifuzu Robo Fainali
Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amewaambia wadau wote wanaoitakia mema timu hiyo kufanya chochote wanachoamini kitasaidia timu yao kupata ushindi kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya MC Alger mchezo ambao utachezwa uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kamwe amesema mchezo huo ni muhimu kwa sababu umeshikilia hatma ya Yanga kwenda hatua ya Robo Fainali na ushindi pekee ndio kitu pekee wanachohitaji dhidi ya MC Alger.