Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imeibua gumzo kubwa baada ya kuwasilisha ombi rasmi la kuwapa uraia wa Tanzania wachezaji wake 9 wa kigeni.
Kulingana Na Maulid kitenge ,barua hiyo, iliyosainiwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Murtaza Ally Mangungu, ilipelekwa kwa Kamishina Jenerali wa Uhamiaji leo, tarehe 23 Januari 2025.
Hatua hii ya Simba imekuja wakati ambapo klabu hiyo inakabiliwa na changamoto za kufuata kanuni za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zinazoweka ukomo wa idadi ya wachezaji wa kigeni wanaoruhusiwa kucheza katika Ligi Kuu.
Uamuzi huo umeibua maswali mengi kuhusu sababu halisi ya ombi hilo na iwapo wachezaji hao wanakidhi vigezo vya kisheria vya kupewa uraia.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, wachezaji hao wanaombewa uraia kwa hoja ya kuwa mchango wao katika maendeleo ya soka nchini ni mkubwa.
Hata hivyo, wachambuzi wa sheria wamehoji uhalali wa mchakato huo, wakisema kuwa unaweza kufungua mlango wa ukiukwaji wa taratibu za uraia.
Simba, kupitia taarifa yao, wameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha ustawi wa klabu yao na kusaidia katika ushindani wa kimataifa.
"Tunaamini wachezaji hawa wanaweza kuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya soka nchini Tanzania," alisema Mangungu.
Hata hivyo, wadau mbalimbali wa michezo na wataalamu wa sheria wameitaka serikali kufuatilia kwa karibu suala hilo ili kuhakikisha kuwa mchakato wa utoaji wa uraia haukiuki sheria za nchi.
Wakati huu, taifa linafuatilia kwa karibu maamuzi yatakayochukuliwa na Idara ya Uhamiaji.
Je, Simba wanapigania haki au wanahatarisha uadilifu wa mfumo wa sheria za uraia? Mu
da utajibu.