Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imewaombea uraia wa Tanzania wachezaji wake 9 ambao sio raia wa Tanzania kupitia barua ya iliyoandikwa kwa Kamishina Jenerali wa Uhamiaji leo tarehe 23 Januari 2025 ambayo imesainiwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Murtaza Ally Mangungu.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally amethibitisha maombi hayo ikiwa ni saa chache baada ya Idara ya Uhamiaji kuwapatia wachezaji watatu wa Singida Black Stars uraia wa Tanzania baada ya wachezaji hao ambao ni Emmanuel Kwame Keyekeh (Ghana), Josephat Arthur Bada (Cote d’lvoire), na Muhamed Damaro Camara (Guinea) kuomba.