Tabora Yapewa Ahadi ya Milioni 50 Wakiikanda Simba


Mkuu wa wilaya ya Tabora Deusdedith Katwale ameweka wazi kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora ametoa ahadi ya TZS Million 50 iwapo wataifunga klabu ya Simba February 2 mwaka huu kwenye dimba la Ali Hassan Mwinyi Tabora.

“Sisi kama Tabora United tunajua kuwa tumecheza nusu fainali kati ya Yanga SC na Tabora United na fainali itakuwa kati ya Tabora United dhidi ya Simba SC. Kwa hiyo kwetu sisi mchezo huu dhidi ya Simba SC utakuwa ni fainali".

"Tushukuru Mungu kuwa tumejiandaa vizuri sana na maandalizi yanaendelea vizuri. Mkuu wa Mkoa ametoa tamko na kutoa ahadi kuwa vijana wetu wa Tabora watakapoifunga Simba SC watapewa zawadi ya milioni 50".

- Deusdedith Katwale, Mkuu wa Wilaya ya Tabora.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad