Elon Musk, tajiri namba duniani anayemiliki makampuni ya Tesla, SpaceX, na X (iliyokuwa Twitter), ameibua mjadala mkubwa baada ya baba yake kuthibitisha nia yake ya kuinunua klabu ya soka ya Liverpool kupitia mahojiano na Times Radio.
Baba yake Musk alieleza kuwa, "Ingawa Elon ameonyesha hamu ya kununua klabu hiyo, haimaanishi kwamba ununuzi utafanyika hivi karibuni." Aliongeza kuwa uhusiano wa familia ya Musk na mji wa Liverpool ni wa kuvutia, kwani mama yake na bibi yake walizaliwa huko, na familia yao ina mizizi ya karibu kwenye mji huo.
Habari hizi zimepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa soka duniani. Wapo wanaoona hili kama fursa nzuri kwa klabu hiyo, huku wengine wakisubiri kuona kama ndoto hii itatimia au la.