Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limetoa ufafanuzi juu ya changamoto iliyotokea na kusababisha kukatika kwa umeme katika maeneo kadhaa ikiwemo katika ukumbi wa Mlimani City wakati Mkutano Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @chadematzofficial ukiendelea.
Kupitia taarifa iliyotolewa na TANESCO leo Januari 21, 2025 imesema chanzo ni hitiliafu katika njia ya umeme ya Mlimani City “Leo majira ya saa 6:56 mchana hadi 6:58 mchana kulitokea hitilafu ya dharura katika njia ya umeme ya Mlimani City kwa muda usiozidi dakika mbili ambapo wataalamu wetu walirekebisha na kurejesha huduma katika eneo hilo kwa haraka.” imesema taarifa hiyo
Taarifa hiyo imeeleza kuwa hali ya upatikanaji wa umeme katika jiji la Dar Es Salaam ni nzuri licha ya kuwepo kwa maboresho ya miundombinu ya umeme katika jiji hilo.
Aidha TANESCO @tanesco_official_page imewahakikishia wateja wake kuwa itaendelea kushirikiana na wadau wote ili kuwezesha shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii.