Tanzania Yapangwa Group B Mashindano ya CHAN 2025
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) leo limechezesha droo ya kupanga makundi ya michuano ya CHAN 2025 ambapo Tanzania imepangwa Kundi B na timu za Madagascar, Mauritania, Afrika ya Kati na Burkinafaso.
Michuano ya CHAN 2025 inachezwa kwa ushirikiano wa Tanzania, Uganda na Kenya na sasa imeahirishwa kutoka kuchezwa February mwaka huu hadi August 2025 kwasababu ya kutoa muda zaidi wa maandalizi kwa Mataifa wenyeji.