Tarehe Mpya za Mashindano ya CHAN Zatangazwa

Tarehe Mpya za Mashindano ya CHAN Zatangazwa


Mashindano ya CAF ya Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024 yanatarajiwa kufanyika Agosti 2-30, 2026.


Kamati ya Utendaji ya CAF (EXCO) inayoongozwa na Rais, Dk. Patrice Motsepe iliidhinisha tarehe hizo mpya wakati wa mkutano uliofanyika Januari 27 huko Rabat, Morocco.


Michuano ya CHAN 2024 itaandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania. Hapo awali mashindano hayo yalikusudiwa kufanyika Februari 1-28, lakini yaliahirishwa.


Katika droo iliyochezeshwa Januari 15, 2025 jijini Nairobi, Kenya ilipangwa Kundi A lenye washindi mara mbili Morocco na DR Congo, pamoja na Angola na Zambia.


Tanzania ipo Kundi B pamoja na Madagascar, Mauritania, Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati,Uganda katika Kundi C ikisubiri kujua wapinzani wengine wawili pamoja na Niger na Guinea.


Wawakilishi wengine kutoka Kanda ya CECAFA Sudan wapo Kundi D pamoja na mabingwa watetezi Senegal, Nigeria na Equatorial Guinea ambao walichukua nafasi ya Congo ambao hawakufuzu kwa kumchezesha mchezaji asiyestahili katika mechi yao ya mwisho ya mchujo.


Mashindano ya CHAN hujumuisha wachezaji pekee wanaocheza ligi zao za nyumbani ikiwa ni katika kuibua vipaji vya wachezaji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad