Dar es Salaam. Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema trafiki walioonekana wakipokea rushwa wakiwa katika majukumu yao ya kazi tayari wameshakamatwa.
Kamanda Muliro amesema hayo leo Jumatano Januari 15, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Video ambayo inasambaa mtandaoni inawaonesha trafiki wakipokea rushwa kutoka kwa makondakta wa daladala.