Tundu Lissu Amchagua Godbless Lema Kuwa Wakala Wake wa Uchaguzi


Tundu Lissu Amchagua Godbless Lema Kuwa Wakala Wake wa Uchaguzi


Mgombea Uenyekiti wa CHADEMA Tundu Antiphas Lissu amemteua aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Kaskazini Godbless Lema  kuwa wakala wake katika mchakato wa ndani wa uchaguzi unaoendelea sasa kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika amewatangazia wajumbe wa mkutano mkuu kuwa Tundu Lissu ametoa taarifa kwa wasimamizi wa uchaguzi kuwa amemteua Lema kuwa wakala wake, na kwakuwa jambo hilo linaruhusiwa hivyo Lema sasa ameingia ukumbini kwa ajili ya kuanza kusimamia kura za Tundu Lissu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad