"Huu ni mkutano wangu wa kwanza wa kichama tangu mwaka 2014, hii ni kwa sababu katika mkutano mkuu wa mwisho wa uchaguzi wa kichama uliofanyika mnamo tarehe 19 Desemba 2019 mimi nilikuwa natibiwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Luven nchini Ubelgiji kufuatia jaribio la mauaji dhidi yangu la tarehe 07 septemba 2017 jijini Dodoma" -Lissu
“Siku hiyo ya 18 Desemba 2019 licha ya kutokuwepo hapa niliwaombeni kura na mkanichagua kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hiki (CHADEMA) kwa upande wa Tanganyika (Tanzania Bara) kwa kunipatia kura asilimia 98.8 ya kura zote halali 941 mlizopiga katika mkutano huo" -Lissu
"Mheshimiwa Mwenyekiti (Freeman Mbowe) nakushukuru sana, na naomab niseme hii hapa kwamba nimekaa pembeni ya Mwenyekiti wetu wa chama kwa miaka zaidi ya 20 na katika kipindi chote hicho hatujawahi kugombana, hatujawahi kuvutana mimi na yeye binafsi, ndio tumetofautiana kimisimamo lakini hatujawahi kugombana, sijawahi kuwa na ugomvi na Mwenyekiti na natumaini hili litaendelea baada ya leo Mheshimwa Mwenyekiti" -Lissu
Salamu za Tundu Lissu @TunduALissu kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA