Tundu Lissu "Namuokoa Mbowe Asije Tolewa Uongozini Kama Mugabe"



Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Bara Tundu Lissu @chadematzofficial na Mtia nia wa nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa amesema moja ya dhamira yake ya kugombea nafasi hiyo ya Uenyekiti ni kuhakikisha anamsaidia Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe kuilinda heshima yake na kutokutolewa madarakani kwa lazima.


Akifanya mahojiano na mtangazaji wa BBC Sammy Awami Lissu amesema “unataka urithi wako uwe urithi wa Mugabe (Robert Mugabe aliyekuwa Rais wa Zimbabwe) anang'olewa huku anasahau kama…unataka urithi wako uwe wa aina hiyo wa watu wakufukuze eee toka toka toka.”


Lissu ameeleza kuwa kwa sasa ili CHADEMA iendelee kutunza heshima iliyoipata kwa muda wote na kuweza kufanya mabadiliko inahitaji nguvu mpya ya kuiongoza na kufikia malengo hayo huku akidai kuwa wa kukiokoa chama ni yeye.


“Mwenyekiti mbowe amekuwa mwenyekiti kwa miaka 21 kwa hiyo kama tunazungumzia kuokoa chama hakiwezi kuwa kinaokolewa na mtu aliyekiongoza kwa miaka 21 inabidi awe mwingine na sehemu ya kugombea kwangu ni kuhakikisha kwamba mwenyekiti analinda heshima yake”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad