Klabu ya Plymouth Argyle inayoshiriki Ligi ya Championship, England imethibitisha kumfuta kazi mkufunzi Wayne Rooney kama kocha mkuu klabuni kwa makubaliano ya pande zote mbili kufuatia mwenendo usioridhisha.
Nyota huyo wa zamani wa Manchester United ameiongoza klabu hiyo kushinda mechi nne, vipigo 13 na sare sita kwenye michezo 23 msimu huu huku klabu hiyo ikiburuza mkia kwenye msimamo wa Ligi hiyo.
Kinara huyo wa magoli wa muda wote wa Manchester United alianza kazi yake ya ukocha baada ya kustaafu kucheza soka akivinoa vilabu vya Derby County, DC United, Birmingham City, na hivi karibuni Plymouth