"Sifa ya kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA sio kuwa umesajili wanachama wangapi, yeye (Shija Shibeshi, mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa) alikuwa 'JOC (Jimbo Operation Commander)' na ilikuwa kazi yake kusajili hao wanachama" -Mahinyila
"Licha ya kwamba mimi nimesema hadharani kuwa hakuna mgombea ninayemuunga mkono, hiyo haina maana kwamba mimi siamini nani anafaa kuwa kiongozi mzuri kwenye chama chetu, na kokote utakapopita nakubaliana na yeye (Shija Shibeshi) vijana wengie wa chama hiki (CHADEMA) wanamuunga mkono Mheshimiwa Tundu Lissu" -Mahinyila
Ni sehemu ya yale aliyosema mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa @bavicha_taifa Wakili Deogratius Mahinyila @AdvMahinyila wakati wa mdahalo wa wagombea hao uliofanyika leo, Jumamosi Januari 11.2024, Dar es Salaam