Vifaa Vya Serikali Shehena za Wizi Zadakwa

Vifaa Vya Serikali Shehena za Wizi Zadakwa


Serikali Mkoani Pwani imekamata shehena ya vifaa vya miundombinu mbalimbali ya Serikali iliyoibwa na kuhifadhiwa katika kiwanda cha kutengeneza vifaa vya ujenzi Mkuranga Mkoani Pwani.


Vifaa hivyo vimekamatwa baada ya kuundwa kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kufuatilia uharibifu wa miundombinu uliokuwa ukifanyika katika Taasisi mbalimbali ikiwemo TANESCO.


Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ameongozana na Viongozi mbalimbali wa Mkoa huo kukagua miundombinu hiyo ambayo imebainika kuwa ni ya Taasisi za TANESCO, DAWASA na Shirika la Reli (TRC) ambapo akiwa katika kiwanda ambacho kilihifadhi vifaa hivyo, RC Kunenge amesema wapo Wananchi wanaisaliti Serikali yao na kuhujumu miundombinu inayosambaza huduma.


Kunenge amesema Serikali imekuwa ikifanya jitihada ya kuboresha miundombinu lakini bado wapo wachache wanaohujumu na kurudisha nyuma maendeleo kwa kufanya uharibifu “Hatutavumilia yeyote atakayehusika kurudisha nyuma maendeleo ya Serikali tutafuatikia tujue nani anayehusika katika hili”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad