Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia Watuhumiwa wawili Fred Rajabu Chaula na Bashir Richard Chaula kwa tuhuma za kula njama na kumuua Regina Rajabu Chaula mwenye miaka 62 Mkazi wa Bahari Beach Wilaya ya Kinondoni na nchini Denmark.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam SACP Jumanne Murilo amesema kuwa Mwanamke huyo alikuwa na kesi za madai Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi dhidi ya Watuhumiwa na Watu wengine na alipotea ghafla na hakuonekana tangu December 13, 2024.
Amesema baada ya ufuatiliaji wa kina katika maeneo mbalimbali na Watu Makachero wa Polisi walilazimika kubomoa shimo la maji machafu ambalo lipo karibu na nyuma aliyokuwa anaishi marehemu na kukuta mwili wa Regina ukiwa umeanza kuharibika.