Watoto wa Familia Moja Watoweka na Dada wa Kazi

Watoto wa Familia Moja Watoweka na Dada wa Kazi


Mohammad Kassim ambaye ni Baba Mzazi, ametangaza kupotelewa na Watoto wake wawili ( wanaoonekana pichani ), ambao wamepotea jana jioni majira ya saa kumi na mbili maeneo ya Temeke Jijini Dar es salaam wakiwa na Dada wa Kazi.


Akizungumza na @AyoTV_, Kassim amesema Dada huyo wa kazi ambaye jana ilikua ni siku ya tatu tangu kuanza kufanya kazi kwenye Familia hiyo, aliondoka na Watoto hao akiaga kuwa anakwenda nao Dukani lakini wakatokomea moja kwa moja.


“Aliowachukua Watoto ni Dada wa kazi aliyekaa nao kwa siku tatu tu, inaonekana kuiba Watoto ndilo lilikua lengo lake kwasababu baada ya kutokomea simu yake haipatikani na hata wale waliomuunganisha kupata kazi kwetu nao simu zao hazipatikani


“Tunaomba yeyote mwenye taarifa za Watoto hawa aende Kituo chochote cha Polisi kilicho karibu nae au anipigie kwa namba yangu 0744-555-574” - Kassim.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad