Nilipo kuwa nawasiliana na Beyoncé kuhusu kushiriki kwenye wimbo wa Brown Skin Girl, nilitaka kufanya bure kwa sababu nilimchukulia kama mshauri na mtu nayemheshimu sana. Hata hivyo, alisisitiza lazima nilipwe,"** alisema Wizkid.
**"Aliniuliza ni kiasi gani ningependa kulipwa, nikamjibu chochote. Nilishangazwa sana alipoamua kunilipa dola milioni 5 (Takriban Billion 12.7 za Kitanzania) . Zaidi ya hayo, aligharamia safari yangu, malazi yangu hotelini, na usafiri wangu nchini Marekani."**
Wizkid pia alionyesha heshima yake kwa Beyoncé kwa kusema: **"Yeye ni malkia ninayemheshimu sana. Ushirikiano huu ulikuwa wa thamani kubwa kwangu, kwani Grammy yangu ya kwanza ilitokana na wimbo huu."**
Wimbo *Brown Skin Girl* pia ulimshirikisha Blue Ivy, binti wa Beyoncé, na ulipokelewa vyema na mashabiki duniani kote.