Zitto Kabwe Amshukia Mrisho Gambo "Nendeni Kwenye Vikao"




Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema vikao vya Kamati ya Fedha na Mipango vya Manispaa, Baraza la Madiwani na Baraza la Ushauri Mkoa (RCC) ni vikao vya kisheria hivyo utetezi wa Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo wa kutohudhuria vikao hivyo hauna mashiko.

Kupitia ukurasa wake wa X, Zitto ame-nukuu habari yenye utetezi wa Gambo akisema “Lakini Mrisho, vikao vya Kamati ya Fedha na Mipango vya Manispaa, Baraza la Madiwani na Baraza la Ushauri Mkoa (RCC) ni vikao vya kisheria, Wabunge wengi haswa wa siku hizi mnadharau sana vikao vya chini na matokeo yake hamfanyi kazi ya uwakilishi vizuri, huu utetezi wako sio”

Zitto amejibu pia hoja ya Mdau wa Mtandao huo aliyeandika Wabunge wengi wanajisahau kutokana na kupita bila kupingwa maana wanaamini Chama dola kitawabeba na laiti kungekuwa na ushindani wa kweli kwenye sanduku la kura wasingekuwa Wazembe........... Zitto akaandika “Sio kujisahau, Wabunge wengi wanadharau vikao vya chini, nilipokuwa Mbunge moja ya vikao nilikuwa nahakikisha sikosi ni RCC, hiki ni kikao ambacho kinakupa sura ya maendeleo ya Mkoa mzima, kuna nyakati kikao kizima nilikuwa Mbunge pekee yangu kati ya Wabunge 8 wa Mkoa”

Utetezi wa Gambo umekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda hapo jana kumtaka Gambo kuachana na siasa za uchonganishi na badala yake ahudhurie vikao vya mipango ngazi ya Halmashauri na vya ngazi ya Mkoa ili kujadili pamoja kuhusu changamoto na suluhu za masuala mbalimbali yanayohusu Mkoa wa Arusha.

Katika utetezi wake kuhusu sakata hilo la jana, Mbunge Mrisho Gambo leo ameibuka na kusema “Mimi sio Mfanyakazi wa Serikali, mimi ni Mwakilishi wa Wananchi, mimi ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mtu ambaye anaweza kutoa taarifa na rekodi kwamba sihudhurii vikao kwa mujibu wa sheria ni Bunge na sidhani kama yeye kwa nafasi yake ni sehemu ya Bunge”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad