Diamond Platnumz KWAKO KIONGOZI:
Kinachoendelea sasa Mitandaoni kupitia maudhui ya kipindi chenu Mashamsham kimekua kama sehemu ya kuniumiza na kunididimiza kisanaa na kiafya ya Mwili Na akili.
Lakini nasema nashukuru na nimeyapokea yote. Nimekua msanii wa taasisi mwenye kasi na mwenye kuipambania kazi yangu licha ya uwekezaji unaofanywa na kampuni yenu sikatai ni jambo kubwa na la kheri kumkomboa binti mwenye kipaji kwa kumuwekezea. Lakini nauliza Je, ni haki hiko kutumika kama silaha kwangu?. Au niliwakosea nini mpaka kufikia kunifanyia Bullying na harassment hizi. Nasibu familia yako wana baya langu lipi ambalo wanaona ni haki wao hata wakiwa na mahojiano binafsi kutokueka stara ya mambo yangu, na huwa wanahakikisha hawakuharibii wewe bali mimi.
Nimefikia hatua leo naandika barua ya kisheria Kwa walezi wangu sababu ya ukandamizaji wa mara kwa mara juu yangu Inauma sana, nitaenda mahakamani na pengine sitaweza kushinda taasisi yenu yenye nguvu lakini hata nikishindwa huko Namuachia MWENYEZI MUNGU yeye ndo Hakimu wa mwisho.
ASANTENI NASHUKURU kwa kuendelea kunibully na kuniharrass. Nishaomba Sana kwako kama kiongozi lakini mara nyingi maombi yangu hugonga mwamba na kunatengenezwa Content za kusudio la kunivunjia heshima, Kuniumiza na kuharibu afya yangu ya akili. Mimi ni binti na mwanamziki pia, sijawahi kuona media yoyote inaniharras kama ambavyo media ya taasisi yenu mmekua mkifanya.
Sina cha kuwafanya kikubwa nyinyi ni wenye Nguvu Na mimi Namshitakia Mwenye Ukuu, utukufu zaidi yangu na ninaenuamini zaidi M/MUNGU .
ASANTENI SANA NASHUKURU 💔