Icrea Cream leo ni tamu sanaaaah
Azam bila mpira muundo wao 4-3-3.Kisha walichagua kufanya mambo ya msingi
1.Kuwatumia runners kwenye mashambulizi ya kushtukiza (Nado& Silha)
2.Kuweka presha kwenye mstari wa katikati mwa uwanja kwa ajili ya kupunguza hatari za Simba kutoka kwa Kagoma+Ngoma +Ahoua.Kwenye hili James Akaminko + Yahya Zaidy walikuwa bora kwenye kuweka presha (Mid Pressing)
3.Nado +Fei Toto + Nassoro Saaduni walikuwa wanaweka presha vizuri kwenye mjengo wa mashambulizi ya Simba (build Up).Goli la Silha ni Matokeo ya presha kwenye mstari kwanza Azama kwenye 4-3-3.
Simba leo wachezaji wawili kwa kiasi kikubwa walihusika kwenye kutengeneza hatari kwa Azam ambao ni Mpanzu + Kibu +Ahoua kivipi?
1.Kibu nguvu na kasi yake ya usumbufu kutokea kwenye mapana ya uwanja na katikati imetengeneza magoli mawili.
2.Mpanzu hasa kipindi cha kwanza alikuwa bora kwenye matumizi ya kasi yake kwenye kuushambulia ule upande wa kushoto kuingia pia ndani (Kufunga goli)
3.Jean Ahoua alikuwa bora kwenye kusaidia build ya Simba kipindi ambacho Azam walionekana wanaweka presha kubwa kwenye mstari wa kwanza kwenye muundo wa 4-3-3.
Zingatia
James Akaminko ni monster kila pafu lake pale katikati liligusa nyansi za uwanja.🔥
Mpanzu muda anawaza kuwapima watu umri.(Kasi +nguvu+ chenga).
Idd Nado anajua sana mpira,Kapombe anafahamu hilo.
Silha mchezaji wa mechi kubwa🔥
Zidane kaifanya vita ya ubingwa kuwa tamu mno.
Full-time
Simba 2-2 Azam