WAAMUZI wa Tanzania Ahmed Arajiga, Kassim Mpanga, Said Hamdani na Salum Nasir wameteuliwa na na Shirikisho la soka Duniani (FIFA) kuchezesha mchezo wa Kundi G wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 kati ya wenyeji Botswana dhidi ya Algeria utakaopigwa Mjini Francistown Nchini Botswana Machi 21, 2025.
Algeria na Msumbiji wapo kileleni mwa Kundi G wakiwa na pointi 9 kila mmoja wakifuatiwa na Botswana, Guinea, na Uganda wenye pointi 6 kila mmoja huku Somalia ikiburuza mkia bila pointi yoyote