Web

Ajali Mbaya ya Gari Mkoani Mbeya, Idadi Waliofariki yatajwa



Ni dhahiri kuwa visa vya ajali barabani nchini Tanzania vimeongezeka hivi karibuni. Jambo ambalo linaendelea kuibua hisia mbalimbali. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, watu watatu wamefariki dunia akiwemo mwandishi wa Habari wa kujitegemea mkoani Mbeya, Furaha Simchimba na wengine saba kujeruhiwa kufuatia ajali Iliyotokea mkoani humo. Ajali hiyo ilihusisha basi la Kampuni ya CRN na gari la serikali STM.

Kulingana na taarifa tulizozipata, ajali hiyo ilitokea siku ya Jumanne Februari 25, 2025 katika eneo la Shamwengo wilayani Mbeya wakati basi lenye nambari ya usajili T599 DZQ likipita gari la serikali lenye nambari ya usajili 6167 bila kuchukua tahadhari na kugongana nje ya baraba na kusababisha vifo hivyo na majeruhi saba akiwemo mwandishi wa Habari wa kujitegemea wa Channel Ten mkoani Mbeya, Epimacus Apolinary, mwenyekiti na katibu wa UWT mkoa wa Mbeya.

Kaimu kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Wilbert Siwa amethibitisha ajali hiyo akieleza kuwa kati ya majeruhi saba wawili kati yao ni mahututi.

Kwa hivyo ongezeko la visa vya ajali za barabarani nchini Tanzania ni uzembe wa madereva na pia adhabu ndogo inayotolewa kwa waliosababisha ajali hizo.




Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad