Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemhukumu Khamis Luwoga (45) adhabu ya kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mkewe, Naomi Marijani, kisha kuchoma mwili wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa.
Hukumu hiyo imesomwa leo, Februari 26, 2025, na Jaji Hamidu Mwanga baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi 14 wa upande wa Jamhuri, waliothibitisha bila shaka kuwa Luwoga alitekeleza mauaji hayo.