Amuua Mzazi Mwenzie na Kutokomea Kusiko Julikana...

Amuua Mzazi Mwenzie na Kutokomea Kusiko Julikana...



Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamtafuta Abdallah Mohammed miaka 40, fundi Frijl mkazi wa Mataya Kata ya Kiromo, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani kwa tuhuma za Mauaji ya mzazi mwenzake Naomi Mwakajengele maarufu kwa jina la Anangisye miaka 28 mwalimu wa Shule ya Msingi Mataya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani imesema kuwa tukio hilo Iilitokea Februari 10, 2025 saa nane usiku ambapo wawili hao wakiwa chumbani kwao zilisikika kelele toka kwa marehemu Naomi Mwakajengele akidai mwenza wake anamuua ndipo, baada ya muda Mohammed ambaye kwa sasa ni mtuhumiwa alitoka ndani na kwenda chumba cha dada wa kazi na kumtaka kulala na watoto wao wawili mwenye umri wa miaka minne (4) na mwengine wa miaka miwili ambao awali walikuwa wamelala na marehemu mama yao.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Dada wakazi alishtuka asubuhi baada ya jirani alipokuwa akimuita Mohammed huku mlango ukiwa wazi pasi na kufahamu baba wa nyumba aliondoka muda gani kwenda kusikojulikana.

“Uchunguzi wa awali umebaini mwili wa marehumu kuchomwa na kitu chenye ncha kali ubavu wa kulia, ubavu wa kushoto na kwenye chembe ya moyo. Awali walikuwa na tofauti ambazo zilipelekea kutokuishi pamoja kwa muda mrefu wawili hao, kabla ya Mohammed kurudi tena kwa mzazi mwenzie wiki mbili zilizopita na kutokea kwa tukio hilo,” imeeleza taarifa hiyo

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limesema linatoa wito kwa yeyote atakaemuona mtuhumiwa huyo kutoa taarifa mapema kwa Jeshi hilo, viongozi wa Serikali au chombo chochote cha dola ili aweze kukamatwa na hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad